C. SHUGHULI ZA KISWAHILI
UMUHIMU WA KULA MATUNDA

Katika picha hii kuna matunda ya kila aina. Matunda haya ni kama nanasi, tikitimaji, papai, ndizi, tundadamu, chungwa, embe, tofaha na mengine mengi. Matunda hukinga miili yetu kutokana na magonjwa. Mtu asipokula matunda atakuwa akiugua mara kwa mara. Matunda kama mapapai na maembe husaidia sana kwa macho. Ni vizuri kuhakikisha kuwa tunakula matunda kila siku ili tusiwe wagonjwa.
1. Matunda hutusaidia kwa ____