GREDI YA 6. KAZI YA LIKIZO, APRILI 2024
SHUGHULI A KISWAHILIMAJADILIANOVIUNGO VYA MAPISHI
Je, unaweza kuvitambua viungo hivi vya mapishi katika picha hii?
Soma majadiliano haya baina ya mama na mtoto wake kisha ujibu maswali.MTOTO: Shikamoo mama.
MAMA: Marahaba mwanangu, umeshindaje?
MTOTO: Nimeshinda vyema mama. Shuleni tumesoma mengi.
MAMA: Ahsante mwanangu. Jitahidi! Jitahidi sana!
MTOTO: Mama, mwalimu wetu wa Kiswahili ametupa kazi ya kuvijua viungo vya mapishi. Amesema tusaidiwe na wazazi.
MAMA: Sawa, chukua kitabu basi uandike.
MTOTO: Ahsante mama. Niko tayari.
MAMA: Tutaanza kwa kitunguu. Kuna kitunguu maji, kitunguu viazi na kitunguu thumu ama saumu. Pia kuna pilipili za aina nyingi. Kuna kichaa, pilipili manga, pilipili boga na pilipili za kawaida.
MTOTO: Pilipil hoho ni gani mama?
MAMA: Pilipili hoho ni ndogo ambazo huwa kali zaidi. Nazo pilipili boga huwa kubwa, mara nyingi za kijani wala si kali hata kidogo.
MTOTO: Mama hizo kubwa ndizo huitwa hoho.
MAMA: Hapana mwanangu. Hayo ni makosa. Hoho ni kali sana na ndogo kabisa.
MTOTO: Mwalimu alisema kuna tangawizi. Hiyo ni nini?
MAMA: Tangawizi ni kiungo kitachotiwa katika chai au chakula. Huwa kinasababisha ladha tamu na ni dawa pia. Pia kuna ndimu. jira, nyanya, bamia, halwaridi ya chai, kuna bizari, iliki, karafuu, mdalasini na masala. Viungo ni vingi mwanangu.
MTOTO: Mama unajua vingine? Nataka kujua zaidi. Mwalimu wetu anapenda wanafunzi wanaojitahidi sana kufanya kazi ya ziada.
MAMA: Aah! Vilevile kuna manjano, kungumanga, zabibu kavu, mrihani, giligiliani hata uwatu.
MTOTO: (
Akicheka sana)Mama manjano ni rangi si kiungo cha chakula.
MAMA: Pia ni kiungo cha chakula ambacho wazungu huita
tumeric. Ni kizuri sana kwa kusafisha damu na kutunza figo.
MTOTO: Aah! Kumbe mama unajua viungo vingi hivyo! Ahsante sana kwa kunisaidia. Mwalimu wetu atafurahi sana.
Hewala mwanangu. Sasa acha nikanunue dania nayo nipikie mchuzi.
MANENO MAPYA.
Tumia kamusi yako utafute maana ya maneno haya.
- tangawizi
- mdalasini
- iliki
- karafuu
- jira
- giligiliani
- manga
- kungumanga
- hoho
Jibu maswali haya.
1. Ni kiungo kipi kati ya hivi utatia katika chai?