SHUGHULI ZA KISWAHILI GREDI YA 3.
MADA KUU : UZALENDO
MADA NDOGO : MSAMIATI WA UZALENDO.
Tazama kwa makini picha hizi.

Nchi yetu ya Kenya.

Mkenya mzalendo.

Kiatu chenye rangi za bendera ya Kenya.
- Je, picha ya kwanza inaonesha nini?
- Picha ya pili ina mtu aliyevaa kibarakoa cha aina gani?
- Ungependa kuvaa kitu chochote chenye rangi za bendera yetu?
SOMA SENTENSI HIZI.
- Nchi ni taifa la watu.
- Watu wanaoishi katika nchi fulani huitwa wananchi.
- Wananchi pia huitwa raia.
- Mtu anayeipenda nchi yake huitwa Mzalendo.
- Wananchi wakiwa wazalendo huishi kwa amani bila vita.
- Amani huletwa na upendo.
- Umoja ni kuishi kwa upendo na watu wote na kufanya kazi nao.
- Umoja na amani huleta maendeleo.
- Bendera ni ishara ya umoja wetu.
- Je, unajua maana ya rangi za bendera yetu? Mwambie mzazi akuelezee.
SHUGHULI YA KUANDIKA:JIBU MASWALI.1. Sehemu wanakoishi wananchi huitwa _____