Welcome to your KISWAHILI 6..
KISWAHILI DARASA LA 6.TAMATHALI ZA LUGHATASHBIHI.Tashbihi ni mbinu ya kulinganisha kitu kimoja na kingine ukitumia maneno kama vile kama na mithili ya.Tunapolinganisha kitu huwa tunatafuta kingine chenye sifa kama zile tunazotaka kutumia. Kwa mfano, tukitaka kusema kitu ni kizito, tutasema ni kizito kama nanga. Tukitaka kusema ni chepesi tutasema ni chepesi kama unyoya.Tazama nanga na unyoya.Hii ndiyo nanga.Mifano ya sentensi.1. Mama amebeba mzigo mzito kama nanga2. Kifaru ni gari zito kama nanga.Huu ni unyoya. Unyoya ni mwepesi sana. Tunasema kitu ni chepesi kama unyoya.Mifano:1. Mzigo wa baba ni mwepesi kama unyoya.2.Simu ya mwalimu wetu ni nyepesi kama unyoya.Mifano zaidi ya tashbihi1. mwema kama mzazi2. mrefu kama mlingoti3. mzuri kama hurulaini4. mweusi kama mpingo/kizimwili5. mjinga kama samaki/kondoo6. mnene kama nguruwe7. mkondefu kama sindano/ ng'onda8. mvumilivu kama mtumwa9. baridi kama barafu10. Eupe kama bafta/thelujiZOEZI: KAMILISHA KWA TASHBIHI ZIFAAZO.1. Suleimani ni mkaidi kama ______
2. Amina ana bidii kama _____
3. Mwalimu wetu ni mpole kama ______
4. Muthoni na Atieno wanapendana kama __________
5. Idi ni mtoto mwenye kelele kama____
6. Kwao na kwetu kumetengana kama ___________
7. Kijana huyu aliadhibiwa na mwalimu kwa kuwa mnafiki kama____
8. Maria ni mwoga kama ____
9. Rangi ya nguo ya shangazi ni nyekundu kama_____
10. Mgeni aliyekuja kwetu alikuwa na shingo ndefu kama ____
Time's up
Your email address will not be published. Required fields are marked *
Comment *
Name *
Email *
Website
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ