Welcome to your KISWAHILI 8.
SOMO LA KISWAHILIKAULI YA KUTENDESHATazama picha hii. Mwalimu anafanya nini?Kauli ya kutendesha huonesha mtu akifanya mtu mwengine afanye jambo, au kitu kikifanya kingine kifanye jambo. Katika picha hii, mwalimu anawafanya wanafunzi wasome, kwa hivyo anawasomesha.Kauli ya kutendesha ina jinsi sita kama ifuatavyo:1. Kitenzi huishia kwa -sha soma - somesha pika - pikisha andika - andikisha2. Kitenzi huishia kwa -za fanya - fanyiza penda - pendeza oa - oza3. Kitenzi hushia kwa -vya lewa - levya nawa - navya lowa - lovya4. Kitenzi huishia kwa -fya ogopa - ogofya ongopa - ongofya5. Kitenzi huishia kwa -sa tokota - tokosa nata - nasa 6. Kitenzi huishia kwa -nya gawana - gawanya pona - ponya MASWALI.Jaza mapengo katika sentensi hizi kwa kutumia kitenzi katika kauli ya kutendesha.1. Siti Maria alim_____ mtoto kitandani alipolia.
2. Wazee wamekanywa kuwa______ binti zao wakiwa wadogo.
3. Ni vizuri kuwa_______ watu umuhimu wa masomo.
4. Mama alim_______ mwanawe mti kwa shoka butu.
5. Ni nani alim______ paka wetu majini?
6. Si vizuri kum_______mnyama yeyote.
7. Mwalimu alitu______ kulaza damu darasani.
8. Mbwa wa Thuranira wana________ sana.
9. Pombe _______
10. Mwanaskauti ame_______ bendera vizuri.
Time's up
Your email address will not be published. Required fields are marked *
Comment *
Name *
Email *
Website
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ