KISWAHILI DARASA LA 8
SOMO : KAULI YA KUTENDEKA.
Tazama picha hizi.
(i) Huyu ni mzee Thuranira. Mzee Thuranira amelima shamba lake ili apande viazi. Shamba hili limelimwa likalimika.
(ii) Huyu ni mam Sein. Mama Sein amepika chakula kitamu sana. Chakula kimepikwa kikapikika.
Kauli ya kutendeka huonyesha kuwa kitendo kimefanyika. Kwa hivyo ni lazima kitendo kiwe kimefanywa ili nacho kifanyike.
Ikiwa kitendo huishia kwa irabu au vokali (a,e,i,o,u) mnyambuliko wa kitendo hicho hubadilika na kuongezea l. Hapa pana mifano miwili ya minyambuliko hiyo.
A
i) lima - limika
ii) pika - pikika
iii) piga - pigika
iv) osha - osheka
v) imba - imbika
B
i) tia - tilika
ii) oa - oleka
iii) lea - leleka
iv) tii - tiilika
v) pokea - pokeleka.
JIBU MASWALI HAYA KWA KAULI IFAAYO YA KUTENDEKA.
1. Kemboi alikimbia mbio za masafa marefu___