KISWAHILI DARASA LA 8
MADA: MAJINA YA WAFANYAKAZI MBALIMBALI

Tazama kwa makini picha hii. Unaweza kuwatambua nani na nani?
SOMA KIFUNGU HIKI.
Katika mahakama kuna watu mbalimbali ambao hufanya kazi mbalimbali. Jaji au hakimu hutoa uamuzi wa kesi. Wakili hutetea mshtaki au mstakiwa. Pia kuna kiongozi wa mashtaka ambaye huyaongoza mashtaka yote. Karani wa korti huapisha watu na kuweka rekodi za mahakama. Iwapo mtu hajui lugha fulani, basi kuna mkalimani au mtapta ambaye hutafsiri lugha mahakamani. Msajili wa Mahakama huandikisha na kuhifadhi kesi zote mahakamani. Baada ya mahakama kumaliza kesi zake za siku topasi au mfagizi huingia na kuosha kila pahali. Je, unawajua wafanyakazi wengine gani?
Tazama orodha hii ya wafanyakazi na utafute kazi wafanyazo.
- Mwashi
- mhasibu
- mwalishi
- mpishi
- yaya
- kijakazi/kitwana
- mnyapara
- mpakizi
- msusi
- mkunga
- tarishi
Jibu Maswali haya.1. Mtu anayetumwa kupeleka ujumbe wa posa huitwaje_______