STD 5 KISWAHILI

STD 6 SOCIAL STUDIES
November 12, 2020
STD 6 C.R.E
November 14, 2020

STD 5 KISWAHILI

Welcome to your STD 5 KISWAHILI

KISWAHILI DARASA LA 5

NOVEMBA 2020.


MADA: KIULIZI PI?

TAZAMA SENTENSI HIZI
 Kiulizi pi huandamana na ngeli ya neno.
Ni mtoto yupi aliyechelewa kuingia darasani?

  • Ni kitabu kipi kilichopotea?
  • Ni sahani ipi imevunjika?
  • Chupa zilizoanguka ni zipi?
  • Gari la baba ni lipi?
  • Mkoba uliopotea ni upi?
  • Vyombo vilivyoibwa ni vipi?

SASA JIBU MASWALI YAFUATAYO KWA KIULIZI ~PI?
1. Ni mgonjwa __________ aliyepelekwa hospitalini?

2. Ni meza _______ ambayo imefunikwa?

3. Maziwa yaliyopikiwa chai ni ___________?

4. Ni ndege _________ ametaga mayai haya?

5.  Vyuma vilivyotengenezewamadirisha ni _______?

6. Ni msafara _______ ambao ni wa magari ya rais?

7. Ni kipindi _________ husomwa Kiswahili?

8. Ni wanyama ________ hupatikana mbuga ya Tsavo?

9. Ni rais _______ aliyeongoza Kenya vizuri?

10. Ni pahali ________ palipopandwa mboga za majani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WeCreativez WhatsApp Support
One of our Teachers is here. Ask for help
Hi, how can I help