STD 6 MATHEMATICS..July 14, 2020GRADE 3 ENVIRONMENTALJuly 15, 2020 0 GREDI YA 5… KISWAHILI Welcome to your GREDI YA 5... KISWAHILI Name Class Phone KISWAHILI GREDI YA 5MADA : KUFAHAMUSOMO : MICHEZOMwogeleaji akiwa tayari kupiga mbizi.SOMA KIFUNGU HIKI.Michezo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Michezo husaidia sana mwili katika mambo mengi. Je, wewe unapenda kucheza? Unajua mchezo wowote? Michezo ni ya aina nyingi. Kuna michezo kama vile kuogelea, kucheza soka au kandanda, kuruka urefu,mpira wa nyavu, mpira wa vikapu, mpira wa magongo, jugwe, mbio za magari, kuendesha farasi, riadha na pia kuna michezo ya watoto kama vile nage, foliti na gungwe. Michezo ina faida nyingi sana. Kwanza michezo hunyoosha viungo vya mwili na kufanya mwili kuwa mwepesi, Pili, michezo hupunguza uzito na kumpa mtu afya bora. Tatu, michezo hupumzisha akili baada ya kuchoka. Vile vile michezo huleta watu pamoja. Michezo pia huleta riziki. Marefu na wanasoka wengi hupata pesa kutoka michezoni. Je, unajua faida nyingine yoyoyte ya michezo? Msamiatii) Jugwe - mchezo wa kushindana kuvuta kamba.ii) Nage - mchezo wa kulenga watu na mpira na kujaza mchanga chupani.iii) foliti - mchezo wa watoto wa kufukuzanaiv) gungwe- mchezo wa kurukaruka kwa mguu mmoja.v) mwajificho - mchezo wa watoto wa kujificha na kutafutana.vi) Refa- mtu anayeamua mchezo uwanjani, mwamuzi.vii) Riziki - chakula.MASWALI.1. Mchezo wa kupiga mbizi ni sawa na _______ kucheza soka kuruka kuogelea None 2. Mpira wa nyavu ni sawa na ______ voliboli netiboli nage None 3. Mchezo wa watoto wa kujificha na kutafutana huitwaje? mwajificho nage gungwe None 4. Mchezo unaochezwa kwa kifaa hiki huitwa mchezo wa_______ kabumbu magongo nyavu None 5. Mtu anayetoa maamuzi uwanjani huitwaje?_____ refa mchezaji mtazamaji None 6. Ni ipi si faida ya michezo? kunyoosha viungo kupata chakula kuuza mali None 7. Ni mchezo upi ambao watu wawili hupigana ngumi? soka ndondi gofu None 8. Kando na kufurahia, michezo pia _____ hufanya watu wapigane inaleta wizi hujenga mwili None 9. Mchezo wa watoto wa kulengana na mpira na kujaza mchanga chupani ni ____ nage foliti gungwe None 10. Kunyoosha viungo mtu anapocheza husaidia mwili _____ kuongeza uzito kurembeka kusafirisha damu vizuri. None Time's up Wanto Leave a Reply Cancel replyYour email address will not be published. Required fields are marked *Comment * Name * Email * Website Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment. Δ