Welcome to your GREDI YA 5... KISWAHILI
KISWAHILI GREDI YA 5MADA : KUFAHAMUSOMO : MICHEZOMwogeleaji akiwa tayari kupiga mbizi.SOMA KIFUNGU HIKI.Michezo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Michezo husaidia sana mwili katika mambo mengi. Je, wewe unapenda kucheza? Unajua mchezo wowote? Michezo ni ya aina nyingi. Kuna michezo kama vile kuogelea, kucheza soka au kandanda, kuruka urefu,mpira wa nyavu, mpira wa vikapu, mpira wa magongo, jugwe, mbio za magari, kuendesha farasi, riadha na pia kuna michezo ya watoto kama vile nage, foliti na gungwe. Michezo ina faida nyingi sana. Kwanza michezo hunyoosha viungo vya mwili na kufanya mwili kuwa mwepesi, Pili, michezo hupunguza uzito na kumpa mtu afya bora. Tatu, michezo hupumzisha akili baada ya kuchoka. Vile vile michezo huleta watu pamoja. Michezo pia huleta riziki. Marefu na wanasoka wengi hupata pesa kutoka michezoni. Je, unajua faida nyingine yoyoyte ya michezo? Msamiatii) Jugwe - mchezo wa kushindana kuvuta kamba.ii) Nage - mchezo wa kulenga watu na mpira na kujaza mchanga chupani.iii) foliti - mchezo wa watoto wa kufukuzanaiv) gungwe- mchezo wa kurukaruka kwa mguu mmoja.v) mwajificho - mchezo wa watoto wa kujificha na kutafutana.vi) Refa- mtu anayeamua mchezo uwanjani, mwamuzi.vii) Riziki - chakula.MASWALI.1. Mchezo wa kupiga mbizi ni sawa na _______
2. Mpira wa nyavu ni sawa na ______
3. Mchezo wa watoto wa kujificha na kutafutana huitwaje?
4. Mchezo unaochezwa kwa kifaa hiki huitwa mchezo wa_______
5. Mtu anayetoa maamuzi uwanjani huitwaje?_____
6. Ni ipi si faida ya michezo?
7. Ni mchezo upi ambao watu wawili hupigana ngumi?
8. Kando na kufurahia, michezo pia _____
9. Mchezo wa watoto wa kulengana na mpira na kujaza mchanga chupani ni ____
10. Kunyoosha viungo mtu anapocheza husaidia mwili _____
Time's up
Your email address will not be published. Required fields are marked *
Comment *
Name *
Email *
Website
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ