SHUGHULI ZA KISWAHILI GREDI YA 2
MADA KUU: SHULENI.
MADA NDOGO : SARUFI
SOMO : MATUMIZI YA ~ako NA ~enu.


Tazama picha hizi. Picha ya kwanza ina mwanafunzi mmoja.
Picha ya pili ina wanafunzi wawili.
Kama mwanafunzi wa kwanza yuko karibu basi utamwambia;
>kalamu hiyo ni yako
>ufutio huo wako
>miwani ile ni yako
>dawati hilo ni lako.
Katika picha ya pili, kama wanafunzi hao wako karibu na wewe, utawaambia;
>vitabu hivyo ni vyenu
>Kalamu hizo ni zenu
>Mikoba hiyo ni yenu.
~ako hutumiwa kuambia mtu aliye karibu na wewe kwamba kitu ni chake, ni yeye mwenyewe.
~enu hutumiwa kuambia watu walio karibu na wewe kuwa kitu au vitu ni vyao, ndio wenyewe.
FANYA MASWALI HAYA.
1. Kalamu ______ iko wapi?