Welcome to your KISWAHILI 6
KISWAHILI DARASA LA 6MADA KUU: TAMATHALI ZA LUGHAMADA NDOGO : TANAKALI ZA SAUTI.i)Huyu ni Bwana Ismael. Bwana Ismael ameanguka pu! Ana maumivu sana.ii)Hili ni gari la polisi. Limetokea na kumulika waa! Kila mtu ametoroka.iii)Huyu ni Irungu. Irungu ni mwogeleaji stadi. Sasa ataruka majini chubwi!Tanakali za sauti ni sauti inayotokea wakati kitendo fulani kimefanyika. Mifano zaidi ni kama :1. Shilingi kuanguka sakafuni tang'!2. Cheka kwa kwa kwa!3. Lia kwi kwi kwi!4. Funga mlango ndi!5. Anguka mchangani tifu!6. Zaba kofi pa!7. Kula fyu!8. Nuka fee!KAMILISHA SENTENSI HIZI,1. Maua yaliyoletwa na baba yananukia ______
2. Saida alimwaga maji _______ karibu animwagie.
3. Leo jua ni kali sana. Limewaka_______
4. Usiondoke hapo ulipo. Tulia ______!
5. Viatu vyangu vya shule ni vyeusi ______!
6. Mama amenunua leso nyeupe ______ kama pamba.
7. Usipofanya kazi vizuri hutapewa chochote ____!
8. Leo sipandi gari lolote. Nitaenda nyumbani_________!
9. Mtoto huyu anapenda kupiga kelele __________ hata huwezi kusikia.
10. Matunda yamejaa sokoni _________ huwezi kukosa kununua.
Time's up
Your email address will not be published. Required fields are marked *
Comment *
Name *
Email *
Website
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ