KISWAHILI DARASA LA 6.
TAMATHALI ZA LUGHA
TASHBIHI.
Tashbihi ni mbinu ya kulinganisha kitu kimoja na kingine ukitumia maneno kama vile kama na mithili ya.
Tunapolinganisha kitu huwa tunatafuta kingine chenye sifa kama zile tunazotaka kutumia. Kwa mfano, tukitaka kusema kitu ni kizito, tutasema ni kizito kama nanga. Tukitaka kusema ni chepesi tutasema ni chepesi kama unyoya.
Tazama nanga na unyoya.
Hii ndiyo nanga.
Mifano ya sentensi.
1. Mama amebeba mzigo mzito kama nanga
2. Kifaru ni gari zito kama nanga.

Huu ni unyoya. Unyoya ni mwepesi sana. Tunasema kitu ni chepesi kama unyoya.
Mifano:
1. Mzigo wa baba ni mwepesi kama unyoya.
2.Simu ya mwalimu wetu ni nyepesi kama unyoya.
Mifano zaidi ya tashbihi
1. mwema kama mzazi
2. mrefu kama mlingoti
3. mzuri kama hurulaini
4. mweusi kama mpingo/kizimwili
5. mjinga kama samaki/kondoo
6. mnene kama nguruwe
7. mkondefu kama sindano/ ng'onda
8. mvumilivu kama mtumwa
9. baridi kama barafu
10. Eupe kama bafta/theluji
ZOEZI: KAMILISHA KWA TASHBIHI ZIFAAZO.
1. Suleimani ni mkaidi kama ______