GRADE 3 LITERACY IN KISWAHILI ACTIVITY.
MADA KUU : KUSOMA
MADA-NDOGO : SAUTI ZINAZOTAMKWA PAMOJA
MB NA ND

Huyu ni Susana. Susana anafanya nini?
SHUGHULI YA 1.
Soma hadithi hii.
Jumapili iliyopita, Susana na kaka yake walikuwa wakichunga mbuzi.
Susana alikuwa akiimba wimbo mzuri waliofunzwa shuleni. Ndugu yake alikuwa akiwapa mbuzi wao maji kwa ndoo. Hapo karibu palikuwa na mti uliozaa ndimu nyingi. Mara ndege wengi wakaja katika mti huo. Ndipo ndugu yake Susana akakimbia na kuchukua jiwe akawarushia. Wakaruka wakaenda. Susana hakupenda hivyo.
Mwambie mzazi wako au mlezi akusaidie kusoma maneno haya mkizingatia kutamka Mb na Nd.
i) mbuzi
ii) imba
iii) wimbo
iv) ndugu
v) ndoo
vi)ndimu
vii) ndege
viii) kimbia
ix) enda
x) penda
SHUGHULI YA 2.
JIBU MASWALI HAYA.
1. Nyumbani kwetu ni _______ na shuleni.