MUHULA WA PILI 2020. KISWAHILI
VITATE
Vitate ni maneno yanayotatanisha wakati yanapotamkwa. Maneno ya vitate huwa na maana tofauti kabisa.
Mifano:
1. a) Mchuzi - chakula chenye supu kinacholiwa kwa kingine.
b) Mchuuzi - Mfanyabiashara anayeuza bidhaa rejareja.
2. a) Nchi - Taifa la wananchi
b) Inchi - kipimo cha urefu wa centimeta mbili na nusu.
3. a) Bawabu - Mtu anayekaa mlangoni ila kulinda
b) Bawaba - Vifaa vinavyoshikilia mlango usianguke.
4 a) Mjusi - Mnyama mdogo wa jamii ya kenge
b) Mjuzi - Mtu ambaye ni bingwa wa kufanya mambo
5. a) Vua - toa samaki majini
b) Fua - osha nguo kwa sabuni na maji.
ZOEZI.
1. Baba alituamuru twende shambani tukang'oe ______