KISWAHILI 8

KISWAHILI 6
September 16, 2020
STD 6 ENGLISH
September 17, 2020

KISWAHILI 8

Welcome to your KISWAHILI 8

Name
Class
Phone

KISWAHILI DARASA LA 8.

MADA: SARUFI

MADA NDOGO: Mkato wa maneno yenye Sauti nne.

Ukuzaji wa mboga mseto za kienyeji Nairobi unampa mapato ya kuridhisha – Taifa Leo
Huyu ni Mama Kasioki. Mama Kasioki anavuna mboga za majani katika shamba lake. Shambale ni kubwa sana. Anataka kupika ugali ale na wana wake. Wanawe wakimaliza kula wataenda kucheza. Mama naye atavua kanga yake ili aifue. Kangaye ikikauka, atajifunga tena. Watoto wasipocheza vizuri wataumizana. Kweli asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimengu.

Maneno yaliyo angaziwa ni mkato wa maneno yenye sauti nne.

  • Shamba lake - shambale
  • Mama yake - mamaye
  • Kanga yake - kangaye
  • Wana wake - wanawe

Katika kukata sauti nne, onatoa sauti mbili za katikati kisha unaunganisha mbili zinazobaki.  Kwa mfano
  • Kalamu Yake - kalamuye
  • Gari lake - garile.

Hata hivyo, kimilikishi wako hukatwo na kubaki o pekee.
  • Mwana wako - mwanao.

NB: Vimilikishi vyenye maneno matatu havifupishwi. Mfano
  • yao
  • pao
  • lao        -   hubaki vivyo hivyo.

MASWALI. Fupisha maneno yaliyoangaziwa katika sentensi.
1. Baba yake Juma ni kandawala.

2. Kila mwanafunzwi anafaa kukaa pahali pake.

3. Mari na dada zake wameenda mtoni.

4. Kesho ukienda kwa babu yako umsalimu sana.

5. Naona kama nguo zako zote hutoka India.

6. Maisha yako unayatakiaje?

7. Wazee wanaooza binti zao wadogo watatiwa ndani.

8. Mbona mwana wako hapendi ushauri?

9. Maseremala hawajamaliza kuunda meza zake Ali.

10. Mwana wao hajaoenekana tangu juzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WeCreativez WhatsApp Support
One of our Teachers is here. Ask for help
Hi, how can I help