ZIADA YA LIKIZO YA APRILI 2021, DARASA LA 7.
LET US TAKE A MINUTE AND CONGRATULATE OUR CLASS 8 2020 FOR GOOD PERFORMANCE. WELL DONE.
408
405
403
383
374
370
370
365
362
359
357
355
355
351.......
The list continues........33 Over 300 marks. We thank God.
KISWAHILI.
MADA: KUSOMA NA KUFAHAMIKIWA
SOMO UFAHAMU.
Tazama picha hii. Unafikiria ni shughuli gani inayoendelea?Je, shule yenu ishawahi kushiriki katika shughuli kama hii?SOMA UFAHAMU UFUATAO Ilikuwa siku ya matembezi ya kukusanya pesa kwa ajili ya wagonjwa wa maradhi sugu yasiyopona.Wanafunzi wa shule ya upili ya Kiria-ini ambao walikuwa wamejisajili kwa shughuli hiyo walijitayarisha mapema. Walikuwa watembee mwendo wa kilometa nane kutoka shuleni kisha warudi kuko huko.
Hii iliwabidi kutoka mapema yapata mwendo wa saa tatu asubuhi. Takriban wanafunzi themanini ndio waliopata nafasi. Lulu na Nikko walikuwa miongoni mwao. Matembezi hayo yalisimamiwa na walimu wanne; wawili wa kike na wawili wa kiume. Bi. Neema alikuwa mmoja wao.
Baada ya kupewa mashauri na kuelekezwa kuhusu matembezi hayo, wote waliondoka shuleni kwa pamoja wakielekea kituoni ambapo walipewa fulana zenye maandishi kuhusu matembezi hayo. Kutoka hapo walitembea pamoja hadi walipoanza kufumukana kwa makundi makundi. Wale waliokuwa wepesi waliongoza wengine huku watepetevu wa kutembea wakisumbukia hali zao.
Jua la mtikati liliwapata taraa walipowasili kwenye kituo cha mwisho ili wageuke waanze kurudi.Hapo ilikuwa watue kwa muda ili kupokea hotuba ya naibu wa waziri wa afya kabla hawajarudi. Wahudumu waliokuwapo kwenye kituo hicho waliwahudumia kwa maji safi pamoja na sharubati angaa wakonge roho. Kwa wale waliolilia dawa za kuwangwa na kichwa, walipewa vidonge vya kutuliza hali hiyo.
Baada ya hotuba fupi kutolewa, wanafunzi waliketi pamoja ili wapewe chamcha.Walimu wawili waliwachukua wanafunzi kadhaa ambao waliwaauni kubeba vilaji. Bila shaka chakula chepesi ni soda na mkate. Aidha kila mmoja aliongezewa yai la kutokoswa na ndizi moja ya mkono wa tembo.
Wakati wakila, Lulu alihama pahali alipoketi na kujiunga na kikundi ambapo Nikko alikuwa. Kilikuwa kikundi cha wavulana watano. Watatu walipomuona waliona izara wakagura kutoka hapo. Nikko alimpokea Lulu wakala pamoja huku wakibadilishana mawazo. Lulu aliamlaumu Nikko kwa kutotembea pamoja naye, naye akajitetea akisema hakupata fursa ya kumuita. Waliahidiana kuwa watakuwa pamoja wakirudi shuleni. Mengi hayakujiri hapo kwani walikuwa sehemu wazi na walimu walikuwa macho sana. Bi Neema hakumaliza zaidi ya dakika tano pasipo kumgeukia Nikko. Pamoja na hayo, wanafunzi wengine walikuwa ange kusikiliza udaku wa wenzi wao na dondoo za mjini.
-Kutoka kitabu 'Mchezo Wa Wanawake' na Wanto Warui.
A. MSAMIATI.Tumia Kamusi yako kutafuta maana ya maneno haya: - sajili
- bidi
- takriban
- shauri
- fulana
- fumukana
- ~tepetevu
- mtikati
- taraa
- tua
- hudumu
- sharubati
- konga
- wanga
- kidonge
- chamcha
- auni
- kilaji
- tokosa
- izara
- gura
- fursa
- jiri
- ange
- udaku
- dondoo.
JIBU MASWALI YAFUATAYO:
1. Kulingana na aya ya kwanza, _____________