SHUGHULI YA 3: KUSOMA NA KUFAHAMIKIWA.
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
Mzee Ojwang' ni mzee mwenye bidii sana.Yeye hufanya kazi ya useremala. Katika karakana yake, yeye hutengeneza meza, makochi, na vifaa vingine. Yeye hupenda kuvaa bwelasuti ili nguo zake zisiwe chafu. Pia huvaa chepeo kuzuia ukali wa miale ya jua. Ameijenga nyumba yake upande wa kusini mwa shule ya Jahari. Nyumba hiyo ina vyumba kama vile sebule, maliwato, jikoni na vyumba vya kulala. Kila jioni Mzee Ojwang' na familia yake; watoto wawili na mke mmoja hukutana ili kula. Chakula hicho huwa kitamu kama asali. Kila mmoja hunawa kwa maji safi na sabuni kabla ya kula. Watoto husubiri wazazi wanawe kwanza ndipo nao wanawe. Kila mtu hunyamaza akila. Wanaelewa kuwa kuongea na chakula mdomoni ni tabia mbaya. Baada ya kula, wote hunawa.Watoto huondoa vyombo mezani kisha wakamsaidia mama yao kuviosha. Baadaye wao huenda vitandani na kulala fofofo.
MASWALI.
1. Kazi ya Mzee Ojwang' ni ya kutengeneza vitu akitumia______