Welcome to your KISWAHILI 8
SOMO LA KISWAHILI DARASA LA 8.UFAHAMU.KAZI IPEWE NANI?Baada ya kumaliza darasa la nane, Amina hakuweza kuendelea na masomo ya shule ya upili kwani wazazi wake walikuwa wachochole. Aidha pale kijijini pao hapakuwa na mtu aliyejiweza wa kumpa udhamini wa masomo. Kwa kuwa ni lazima maisha yangeendelea, Amina alimuomba baba yake ampeleke katika chuo kimoja cha ufundi kilichokuwa hapo pao kijijini. Ingawa baba yake hakuona kama hilo lilimfaa bintiye, ilimbidi tu kufanya hivyo kutokana na hali ilivyokuwa. Basi Amina alijiunga na chuo hicho cha kazi za mikono na akaingia katika idara ya ujenzi. Pale alifunzwa mbinu mbalimbali za uashi na useremala. Alisomea matumizi ya timazi ambayo hupima wima wa ukuta, pimamaji ambayo ilipima usawa wa mbao, filifili ambayo ni ya kupima sehemu zilizohitajika kuwa na kona zenye nyuzi fulani na mwiko wa mwashi ambao ulipigia lipu. Vilevile, alijifunza kutumia jiriwe, kekee, tindo, bisibisi ya kufungulia misumari ya hesi, jinsi ya kufunga na kukaza parafujo na vifaa vingine vya ujenzi. Baada ya kufanya bidii ya mchwa katika mafunzo hayo, aliweza kumudu kazi mbalimbali za mikono. Alipofuzu akaona ni vyema aendelee na mafunzo zaidi na kupata vyeti vya masomo ya mafunzo hayo. Baada ya kufuzu, alianza kupewa kandarasi za ujenzi mijini na punde si punde akawa ni mtu na chake. Wale waliomdharau alipokuwa akienda chuo cha mafunzo wakaanza kumuinamia na kumnyoshea mkono. Kwa kuwa Amina alikuwa mkono wazi, alimwauni kila aliyetaka msaada wake kijijini pao. Hatimaye kijiji chao kikaanza kuinuka polepole. Akawa mhimili mkubwa katika maendeleo ya watu wa eneo lake. Akaifaa jamii sana nayo jamii ikatambua umuhimu wa bidii kwani mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Aidha hili linadhihirisha kuwa kazi yoyote ile inaweza kufanywa na mwanamume au mwanamke.Msamiati1. Uchochole - hali ya umaskini mkubwa.2. Udhamini - kupata msaada ya kifedha kutoka kwa mtu au shirika.3. Timazi - kifaa cha ujenzi kinachopima wima wa ukuta.4. Kandarasi - kazi ya mkataba anayoichukua mtu ili kuifanya kwa muda fulani.MASWALI.1. Ni kwa nini Amina hakuweza kuendelea na masomo ya shule ya upili?
2. Neno ilimbidi kama lilivyotumika katika taarifa lina maana kuwa___
3. Kifaa cha mwashi cha kupimia usawa wa ukuta huitwaje?
4. Kazi ambazo Amina aliamua kufanya zilikuwa ni kama vile
5. Misumari ya hesi hufungwa kwa kutumia_____
6. Ni kifaa kipi kati ya hivi hakikuingiana sana na kazi za Amina?
7. Amina aliamua kuendelea na mafunzo zaidi hata baada ya kufuzu ili
8. Amina alianza kazi yake ya ujenzi wapi?
9. Maoni ya mwandishi katika ufahamu huu ni kuwa
10. Maoni ya kutaka kujiunga na chuo cha ufundi yalitolewa na nani?
Time's up
Your email address will not be published. Required fields are marked *
Comment *
Name *
Email *
Website
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ