KISWAHILI 5

MATHEMATICS 8
June 19, 2020
SHUGHULI ZA KISWAHILI GREDI YA 2
June 20, 2020

KISWAHILI 5

Welcome to your KISWAHILI 5

KISWAHILI DARASA LA TANO

HOSPITALINI.

  • Hospitali ni pahali ambapo mtu hupelekwa ili apewe matibabu akiwa mgonjwa.
  • Katika hospitali kuna muuguzi ambaye huumpa mgonjwa huduma. Pia huitwa nesi.
  • Mtu ambaye humtibu mgonjwa huitwa mganga, tabibu au daktari.
  • Chumba ambacho wagonjwa hulazwa huitwa wodi.
  • Chumba cha wogonjwa mahututi huitwa sadaruki.
  • Ikiwa mtu anahitaji upasuaji, basi hupelekwa thieta.
  • Kuna sehemu ya hospitali ambayo hushughulikia huduma za dharura kama vile ajali, moto n.k
  • Kipimajoto hutumiwa na daktari ili kupima joto la mgonjwa mwilini
  • Kipimamwili hutumiwa na daktari kupimia mapigo ya moyo.
  • Bandeji humfunga mgonjwa aliyuvunjika kiungo cha mwili.
  • Kuna glavu ambazo wahudumu huvaa mikononi ili wasiambukizwe viini.
  • Ukiwa mtu amevunjika kiungo cha mwili, atahitaji kuchunguzwa kwa uyoka ili kuonekana jinsi alivyovunjika.
  • Siku hizi kila mtu akienda hospitalini anahitajika kuvaa kibarakoa mdomoni ili kujikinga na ugonjwa wa korona.
  MASWALI.
1. Mtu anayewapokea wagonjwa hospitalini na kuwapa huduma ni____

2. Chumba ambamo wagonjwa ambao hali zao za kiafya ni mbaya sana hulazwa huitwa_______

3. Ili daktari ajue hali ya mapigo ya moyo ya mgonjwa atatumia_____

4. Wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka sana hupelekwa katika____

5. Daktari huvaa ____mikononi ili huzuia asiambukizwe na viini.

6. Kifaa cha kukagua viungo ndani ya mwili kwa kupiga picha huitwa eksirei au __

7. Mgonjwa akipelekwa hospitalini imhitaji kulala huko tunasema kuwa ame___

8. Mtu akifa hospitalini atahifadhiwa katika chumba kinachoitwa____

9. Hospitali ndogo inayotoa huduma chache za afya huitwa____

10. Kamilisha methali hii : Gangaganga za mganga______

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WeCreativez WhatsApp Support
One of our Teachers is here. Ask for help
Hi, how can I help