Soma majadiliano haya kati ya utingo na abiria kisha ujibu maswali yafuatayo.
UTINGO: Gari wazi, gari wazi!
ABIRIA: Unafika wapi?
UTINGO: Gari mpaka mjini mama, mbao! Mbao!
ABIRIA: Mbao ndio nini sasa?
UTINGO: Mbao ni ishirini mama.
ABIRIA: Haya sawa, acha niingie.(Akiwa ndani) Mbona hakuna viti na umesema gari wazi?
UTINGO: Huoni viti mama, hivi vimekaliwa na wengine ni nini?
ABIRIA: Na mimi nitaketi wapi?
UTINGO: Kuna mzee anashuka hapa mbele, ngojea (akidai nauli). Lipa nauli yako basi.
ABIRIA: (Akimpa utingo shilingi ishirini).
UTINGO: Mama nauli ni shilingi arubaini.
ABIRIA: Ulisema ni ishirini, ulisema mbao ni ishirini kijana (abiria amehamaki)
UTINGO: Nilisema mbao!Mbao! Kwani mbao na mbao ni ngapi mama?
ABIRIA: Basi mimi sina arubaini, nina ishirini tu.
UTINGO: Basi shuka haraka mama, shuka hapa hakuna gari la bure!
Tazama maana ya maneno haya katika kamusi yako:
- Utingo
- nauli
- abiria
- hamaki
Yatumie maneno hayo kukamilisha sentensi hii kwa usahihi.
21. Msafiri hulipa ______ katika chombo cha usafiri.