Welcome to your KISWAHILI 3..
SHUGHULI ZA KISWAHILI, LITERACY, GREDI YA 3.MADA: KUSIKILIZA NA KUONGEAMADA NDOGO:KUSOMA Soma hadithi hii: JOGOO NA MTOTO MTUNDU.Katika kijiji ka Kamwanya, paliishi familia ya mzee Babu. Mzee babu alikuwa na mke na mtoto mmoja mvulana. Mtoto huyu alikuwa kichwa ngumu. Hakupenda kuambiwa. Alifanya aliotaka. Kwao kulikuwa na kuku wengi. Kulikuwa na jimbi mmoja aliyekuwa hatari kwa kufukuza watu hasa watoto. Basi Mzee Babu alimshauri Kijana wake, Masikio, asimchezee jimbi huyu kwa sababu angemjeruhi. Masikio hakusikia, aliweka masikio yake nta. Siku moja aliwapelekea kuku mahindi bila kuambiwa afanye hivyo. Alipowafungulia kuku tu, yule jogoo alimrukia Masikio na kumuinua juu juu. Alimpiganisha chini kisha akamuinua tena! Ilikuwa balaa. Masikio aliona cha mtema kuni. Kama si Mzee Babu kumuokoa, angeuawa na huyo kuku.MASWALI.1. Familia ya Mzee Babu ilikuwa ya watu wangapi?
2. Mzee Babu na familia yake waliishi kijiji kilichoitwa
3. Mtoto wa Mzee Babu alikuwa kichwa ngumu. Hivi ni kusema......
4. Kijana wa Mzee Babu aliitwa
5. Jina lingine la jogoo katika habari hii ni
6. Unafikiri mama yake kijana huyo wa Mzee Babu aliitwaje?
7. Nani alimwambia Masikio apelekee kuku mahindi?
8. Wakati Masikio alipelekea kuku mahindi, yule jogoo ___
9. Ni methali gani tunaweza kumwambia Masikio?
10. Hadithi hii inatunza
Time's up
Your email address will not be published. Required fields are marked *
Comment *
Name *
Email *
Website
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ