STD 5 KISWAHILI

STD 6 KISWAHILI
September 24, 2020
STD 7 MATHEMATICS
October 3, 2020

STD 5 KISWAHILI

Welcome to your STD 5 KISWAHILI

KISWAHILI DARASA LA TANO.

KUSOMA NA KUJIBU MASWALI YA UFAHAMU.

SOMA HADITHI HII KISHA UJIBU MASWALI.
      
Hapo zamani za kale, sungura na fisi walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. La sungura lilikuwa ndilo la fisi na la fisi lilikuwa ndilo la sungura. Urafiki wao ulikita mizizi mpaka ukaonewa wivu na wanyama wengine.
       Wanyama hawa walijulikana sana na upendo wao ukazidi kukua siku baada ya nyingine. Huenda tabia za wanyama hawa ndizo zilizowaweka pamoja. Sungura alikuwa mjanja sana na kwa sababu ya ujanja wake aliweza kwenda na kutafuta chakula kwa urahisi. Fisi kwa upande mwingine alikuwa mlaza damu na mlafi. Kwa hivyo alifurahia kukaa nyumbani na mkewe wakifanya kazi nyepesi tu.
          Siku moja, sungura alikashirishwa sana na tabia ya fisi ya kumuomba chakula kila mara. Akaamua kumfunza adabu. Akambambia waende madukani kuna chakula kingi cha bure. Fisi akafurahi sana. Wakaenda. Huko madukani, sungura alinunua pombe wakanywa. Kwa ajili ya ulafi wa fisi, alikunywa haraka hadi akalewa chakari!
         Walipokuwa wakienda nyumbani, sungura alimwambia fisi, "Leo nitampiga mke wangu hadi afe. Amekuwa akila chakula ananimalizia kila wakati!". Fisi naye akaone kweli hata mke wake amekuwa akimmalizia chakula. Akaamua angempiga.      
            Walifika kwa sungura kwanza. Sungura akamwambia fisi akae hapo barabarani asikie jinsi atakavyompiga mkewe. Akaingia na kuchukua ngoma. Akaipiga huku akipiga kelele na matusi. Kumbe mke wake alikuwa amelala usingizi  wa pono! Fisi aliposikia hivyo akakimbia kwake. Akamwamsha mkewe akampiga sana huku akimtukana. Akampiga na kumpiga mpaka akafa.
       

MASWALI
1. Wanyama wanaozungumziwa hapa mwanzoni walikuwa_______

2. Sungura na fisi walikuwa marafiki

3. Urafiki wao ulikita mizizi; yaani ______

4. Wanyama wengine waliwaonea sungura na fisi wivu kwa sababu _____

5. Fisi alikuwa mlafi sana. Ulafi ni tabia gani?

6. Kulaza damu ni ______

7. Fisi alilewa chakari haraka kwa sababu _____

8. Ni kweli kusema kuwa....

9. Mke wa sungura alikuwa amelala usingizi wa pono. Usingizi wa poni ni ____

10. Maoni ya mwandishi katika hadithi hii ni kuwa...

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WeCreativez WhatsApp Support
One of our Teachers is here. Ask for help
Hi, how can I help