KISWAHILI DARASA LA 6
MADA: SARUFI
MADA NDOGO: KIREJESHI AMBA
Kirejeshi amba hutumika pamoja na virejeshi vyo "O" kulingana na ngeli. Tazama mifano hii hapa chini.
- Mtoto ambaye amepika ni wako.
- Watoto ambao wamepita ni wenu
- Kisu ambacho kilipotea ni cha baba.
- Visu ambavyo vilipotea ni vya baba.
- Gari ambalo lilianguka limeondolewa
- Magari ambayo yalianguka yameondolewa.
- Chupa ambayo imevunjika isitiwe chai
- Chupa ambazo zimevunjika zisitiwe chai.
SASA FANYA ZOEZI HILI UKITUMIA AMBA.
1. Daktari ____________ atakutibu ametoka Ulaya.