GRADE 4 KISWAHILI

KISWAHILI 5..
June 28, 2020
KISWAHILI 8,,
June 29, 2020

GRADE 4 KISWAHILI

Welcome to your GRADE 4 KISWAHILI

Name
Class
Phone Number

SHUGHULI ZA KISWAHILI GREDI YA 4, MUHULA WA PILI

SOMO : WANYAMAPORI

Tazama pcha hii.

1. Je, kuna mnyama yeyote unayemjua hapa?             
2. Taja wanyama ambao ushawahi kuwaona kwa macho?
3. Wanyama hawa hupatikana wapi?
4. Kuna wanyama wengine ambao huwako hapa unaowajua?
Huyu ni Simbamarara.

Tazama wanyama wengine hapa zaidi
.Mnyama huyu ni fisi     
Mnyama huyu ni kakakuona.

Huyu huitwa Chui

Huyu huitwa Duma.                                                  
Tazama tofauti zilizopo kati ya Chui na duma. Chui ana madoadoa makubwa, kichwa kikubwa na ni mnene. Duma naye ana madoadoa madogo, kichwa kidogo na macho yenye mistari kama analia na mwili mwembamba.

Wanyamapori wengine.

1. Ngiri - ana meno mawili yanayotokea nje. Pia huitwa nguruwemwitu.
2. Mbwamwitu-mnyama wa jamii ya mbwa, mkali na mwenye masikio makubwa.
3. Kicheche - mnyama mwenye mdomo mrefu anayekula kuku.
4. Kuchakulo - mnyama mdogo anayefukua mahindi shambani na kula.
5. Nungunungu - mnyama mwenye mishale mwilini ya kurushia wengine akijilinda.
6. Mbuni - ndege mkubwa sana wa porini asiyeweza kuruka.

SHUGHULI ZA NYUMBANI.
Mwambie mzazi wako akusaidie kuwatambua wanyamapori zaidi kupitia kwa mtandao wa simu yake.

JIBU MASWALI HAYA.
1. Ndege mkubwa wa porini asiyeweza kuruka huitwa_____

2. Simba mwenye milia au mistari mwilini huitwa____

3. Mnyama mwenye mbio zaidi ya wote huitwa____

4. Nguruwemwitu pia huitwa ______

5. Mnyama wa porini anayefanana na ng'ombe ni______

6. Mimi ni mnyamapori. Ninaishi majini. Mimi ni_____

7. Mnyama anayeitwa tumbili ni wa familia ya _____

8. Wanyamapori huhifadhiwa katika _____

9. Kati ya wanyama hawa ni yupi wa porini?

10. Kuku anayekaa mwituni huitwaje?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WeCreativez WhatsApp Support
One of our Teachers is here. Ask for help
Hi, how can I help