C. SHUGHULI ZA KISWAHILI
Soma habari hii kisha ujibu maswali.
Daktari: Hujambo Salima?
Salima: Sijambo daktari, shikamoo?
Daktari: Marahaba. Karibu katika kituo cha afya.
Salima: Ahsante daktari.
Daktari: Nikusaidie vipi? Unaumwa?
Salima : La, nimekuja kumchukulia ndugu yangu dawa, hana hali.
Daktari: Ndugu yako yuko wapi?
Salima: Yu nyumbani amelala tu.
Daktari: Mbona hamkumleta hospitalini ili apimwe?
Salima: Mama amesema pengine alishiba sana kwani anaumwa sana na tumbo, kutapika na kuendesha.
Daktari: Hiyo ni hatari sana Salima. Nenda umwambie mama amlete ndugu yako hospitalini ili apate vipimo, inawezekana kuwa ana waba.
Salima: Waba ni nini daktari?
Daktari: Kipindupindu.
Salima: Ahsante daktari, naenda. Tutamleta sasa hivi.
Daktari: Karibuni.
1. Mazungumzo haya ni kati ya ...............