KAZI YA ZIADA YA LIKIZO YA MWISHO WA MUHULA WA 1, 2023
SHUGHULI ZA KISWAHILI.
MAAGIZO
1. Fanya kazi yako katika MTANDAO kisha uiandike katika DAFTARI lako la kazi ya ziada.
2. Ukimaliza kufanya kazi MTANDAONI, hapo chini utaona kitufe cha kukabidhi kazi kilichoandikwa 'Submit'. Bofya na baada ya sekunde kazi yako itakuwa imesahihishwa. Tazama matokeo na ufanye marudio ya maswali uliyonoa.
3. Kumbuka utahitaji kuleta kazi iliyofanya daftarini shuleni, shule itakapofunguliwa.
MADA: KUSOMA NA KUFAHAMIKIWA
SOMO: BABA AMFUMBIA BINTIYE FUMBO.
Je, unaona nini katika picha?Hapo zamani za kale paliondokea binti mmoja. Daima, alimlalamikia baba yake kwamba, maisha yake yamejaa mikosi. Kwamba, hakudhani kama angefanikiwa maishani mwake. Alikuwa amechoka kupambana wakati wote. Alikuwa akipata suluhu ya jambo moja, jingine hilo laja. Baba yake alikuwa mpishi mbobevu. Akampeleka binti jikoni. Akachukua sufuria tatu zenye maji. Kila moja akaiweka kwenye moto mkali wa gesi. Sufuria tatu zilipoanza kuchemka, akatia viazi mbatata kwenye sufuria moja, mayai kwenye sufuria nyingine na kahawa kwenye iliyobakia. Akamwonesha bintiye mahali waketi. Hakusema neno lolote.
Ustahimilivu ulimshinda binti. Alijiuliza maswali mengi. Ni nini baba wake anafanya?
Baada ya dakika ishirini, baba yake akayazima majiko hayo. Akavipakua viazi kwenye bakuli. Vivyo hivyo, mayai. Akamiminia kahawa kwenye kikombe.Akamgeukia bintiye, “Mwanangu, unaona nini?” “Viazi, mayai na kahawa,” akajibu kwa hasira.
“Tazama kwa ukaribu,” alisema. “Vishike viazi.” Binti akafanya hivyo. Akaona
viazi vimetepetea. Babaye akamwambia ayachukue mayai na kuyavunja. Alipoyapiga chini, akagundua ni magumu.
Ndiposa, akamwambia apige funda la kahawa. Binti akanywa akishusha pumzi kwa burudani ya ladha yake. Huku akisisimka, akamwuliza
dingi wake, “Baba, hii inamaanisha nini?”
Akamjibu, “Viazi, mayai na kahawa, vyote vimechemshwa kwa kiwango sawa cha moto, lakini, kila kimoja kimeitikia tofauti. Viazi viliingia vikiwa imara, vikatoka vimetepeta. Mayai yameingia yakiwa dhaifu na mepesi kuvunjika, yametoka yakiwa magumu. Ila kahawa ilikuwa ya kipekee sana. Ilipowekwa tu kwenye maji, yenyewe ndiyo iliibadili rangi na ladha ya maji, ikaleta msisimko!” Binti alikodoa macho tu.
“Wewe ni nani?” Baba yake akamwuliza. Binti akashangaa. Hakujua ajibu vipi. Hakuelewa fumbo la baba yake. Angali anajiuliza hadi leo yeye ni mayai, viazi au kahawa!
A. MSAMIATI
Tumia kamusi kutafuta maana ya maneno haya - lalamika
- mkosi
- pambana
- suluhu
- bobea
- mbatata
- ustahimilivu
- pakua
- tepetea
- mimina
- sisimka
- dingi
I) MASWALI.
1. Binti huyu alikuwa akilalamikia nini kwa baba yake?