KAZI YA ZIADA YA LIVU YA MWISHO WA MWAKA, 2021
KISWAHILI
MAAGIZO
1. Fanya kazi yako katika MTANDAO kisha uiandike katika DAFTARI lako la kazi ya ziada.
2. Ukimaliza kufanya kazi MTANDAONI, hapo chini utaona kitufe cha kukabidhi kazi kilichoandikwa 'Submit'. Bofya na baada ya sekunde kazi yako itakuwa imesahihishwa. Tazama matokeo na ufanye marudio ya maswali uliyonoa.
3. Kumbuka utahitaji kuleta kazi iliyofanya daftarini shuleni, shule itakapofunguliwa.
KUSOMA NA KUFAHAMIKIWA.
UFAHAMU Kuna wakati,
Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge wanambuzi wawe wengi na kumuwezesha kuwa mkwasi kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..
Siku moja Abunuwasi akipokuwa akimpeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia. Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilipendeza machoni mwake ila akasema “Kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?” Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale... .
Abunuwasi akamchukua mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwasi alishangaa na akaona bora angekichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana. Akamfunga mbuzi wake pale akarudi.
Aliporudi pale mwanzo kukitafuta kiatu alichokiacha awali, hakukikuta tena. Alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu. Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na ufukara wake kwa sababu ya tamaa yake.
A. MSAMIATI.Tumia kamusi yako kutafuta maana ya maneno haya:
- abunuwasi
- fuga
- pindi
- lengo
- pato
- mkwasi
- malishoni
- pembezoni
- awali
- fukara
- tamaa
I) MASWALI.1. Kulingana na aya ya kwanza____